Tuesday, July 31, 2012
CHEMSHA BONGO NA BIBLE
Mtunzi wa Mtihani: Rulea Sanga
MITIHANI WA MWISHO WA MWEZI JULAI
2012 WA CHEMSHA BONGO NA BIBLE
Unatakiwa
kujibu maswali yote kwa muda wa saa mbili na nusu. Tunaamini utazingatia hilo agizo kwasababu wewe
ni mtumishi wa Mungu.
Majibu yako unaweza kunitumia katika email yangu rumatz2011@yahoo.com.
Angalia muda ulioanza kujibu kwa makini.
Kumbuka hapo ulipo unasimamiwa na Roho Mtakatifu kwahiyo huwezi kufanya jambo lakuangalizia.
Ukiangalizia Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zitakutoa katika chumba chako cha kufanyia mtihani.
Matokeo yako utatumiawa kwa email na utapewa na cheti cha kufanya mtihani.
Kila swali lina maksi 10
Jinsi ya kujibu: Unatakiwa kuchagua jibu sahihi na ukipata andika namba ya jibu na jibu lake kwa kuandika herufi kama ni A, B, au C. Na usiandike swali, wewe tutumie hiyo herufu na namba ya swali.
MASWALI YOTE NI YA KUCHAGUA
Chagua jibu sahihi;
Majibu yako unaweza kunitumia katika email yangu rumatz2011@yahoo.com.
Angalia muda ulioanza kujibu kwa makini.
Kumbuka hapo ulipo unasimamiwa na Roho Mtakatifu kwahiyo huwezi kufanya jambo lakuangalizia.
Ukiangalizia Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zitakutoa katika chumba chako cha kufanyia mtihani.
Matokeo yako utatumiawa kwa email na utapewa na cheti cha kufanya mtihani.
Kila swali lina maksi 10
Jinsi ya kujibu: Unatakiwa kuchagua jibu sahihi na ukipata andika namba ya jibu na jibu lake kwa kuandika herufi kama ni A, B, au C. Na usiandike swali, wewe tutumie hiyo herufu na namba ya swali.
MASWALI YOTE NI YA KUCHAGUA
Chagua jibu sahihi;
- Kitu gani kilitokea wakati Yesu
anabatizwa
(a) Wingu jeusi
(b) Tetemeko la ardhi
(c) Mbingu za dunia zikamfunukia akaona Roho wa Mungu akishuka
kama hua, akija juu yake, na sauti kutoka juu ikisema, Huyu ni
mwanagu mpendwa wangu, ninayependezwa naye
- Yesu alipopandishwa na Roho nyikani ili
ajaribiwe na ibilisi, alifunga kula siku ngapi?
(a) kumi
(b) Sita
(c) Arobaini - (i) Yesu alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akimsihi
akisema, Bwana mtumishi wangu amelala, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu
akamwambia,
(a) Amini ameshapona
(b) Nitakuja, nimponye
(c) Nitakuja, nimuokoe na atapona.
(ii) Yule akijibu akasema, Bwana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno na mtumishi wangu atapona. Yesu aliposikia hayo alistajabu akawambia wale waliomfuata
(a) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
katika Israel
(b) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
katika mkutano huu
(c) Amini na wambie sijaona upendo kubwa kama huu kwa yeyote
katika Israel
- (i) Kuna muujiza ambao Yesu
aliufanya wa kuiongeza mikate na samaki ambapo wanafunzi wake walikula
mpaka wakasaza. Ni mikate mingapi na samaki ngapi ambazo Yesu aliziombea
kwa kutazama juu mbinguni kwa Mungu?
(a) Mikate miwili na samaki watano
(b) Samaki wawili na mikate mitano
(c) Mkate mmoja na samaki waili
(ii) Masazo yaliyobaki baada ya wanafunzi kula na kushiba ilijaa vikapu vingapi?
(a) kumi na viwili
(b) Kuma na saba
(d) viwili
- Ni baada ya kufanya nini, Yesu aliwaambia,
“Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya
kuwa pango la wanyang’anyi”.
(a) Ni baada ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
waliokuwa wanauzia njiwa
(b) Ni baada ya Yesu kuingia msikitini na kuona watu wakiuza na
kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
waliokuwa wanauzia njiwa
(c) Ni kabla ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
waliokuwa wanauzia njiwa - (i) Yuda alipoona ya kuwa Ysu
amekwisha kuhukumiwa, alifanya nini?
(a) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
vipande thelathini na moja vya fedha
(b) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
vipande thelathini vya fedha
(c) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
vipande thelathini vya dhahabu
(ii) Ni maneno gani Yuda alisema baada ya kurudisha vile vipande alivyopewa kwaajili ya kumsaliti Yesu?
(a) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia
(b) Alisema, Sijakosea nilipoisaliti damu isiyo na hatia
(c) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu iliyo na hatia
(ii) Yuda baada ya kukimbia ndani ya hekalu kutokana na kumsaliti Yesu alifanya nini?
(a) Alikimbia na kujinyonga
(b) Alirudi na kumsujudia Yesu
(c) Alihuzunika sana na kulia
- Baada ya kusikia kuwa Herode
amekufa Misri, Yusufu, Yesu na Bikira Maria walitoka Israel
ni wapi walienda kuishi?
(a) Nazareti
(b) Misri
(c) Marekani - Taja majaribu matatu ambayo Yesu
alijaribiwa na Ibilisi nyikani?
(a) (i) Mawe yawe mikate
(ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu
(iii) Kumsujudia Ibilisi
(b) (i) Mchanga uwe mikate
(ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha mlima
(iii) Kumsujudia Ibilisi
(c) (i) Mawe yawe mikate
(ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu
(iii) Kumsujudia Mfalme - Yesu aliposhuka mlimani, makutano
mengi walimfuata. Na tazama akaja mtu mwenye ukoma, akamsujudia akisema,
(a) Bwana ukitaka unaweza kunitakasa
(b) Bwana ukitaka waweza kunibariki
(c) Bwana ukitaka waweza kunihurumia
- (i) Taja jina la mfalme
aliyemfunga na kumtia Yohana Mbatizaji gereza?
(a) Kayafa
(b) Rulea Sanga
(c) Mfalme Herode
(ii) Kwani Yohana alifungwa gerezani?
(a) Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye
Filipo awe mke wake na Herode.
(b) Yohana alimwambia sio halali kwa Kayafa kuwa na nduguye
Musa awe mke wake na Herode.
(c) Majibu ya hapo juu sio sahihi
(iii) Kwanini mfalme alipoona watu akaogopa kumuua Yohana Mbatizaji?
(a) Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye
Filipo awe mke wake na Herode.
(b) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Nabii
(c) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Mfalme
(iv) Ni nani aliyecheza mbele ya Herode wakati wa sikuku yake ya kuzaliwa akampendeza Herode kwa uchezaji wake?
(a) Binti Herode
(b) Mjukuu wa Herode
(c) Rafiki yake na Binti Herode
(v) Ni nani alimshauri huyu mtu aliyecheza mbele ya mfalme Herode na mpaka Herode akakubali kutimiza kiapo chake cha kumpa chochote atakachoomba?
(a) mama yake
(b) Kaka yake
(c) Rafiki yake
(vi) Huyo aliyemfurahisha Herode kwa kucheza aliomba nini apewe na huyo mfalme?
(a) hakuomba chochote
(b) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika mfuko
(c) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika kombe
(vii) Unafikiri Herode alifuarahia ilo ombi la huyu aliyecheza vizuri katika sikuku yake ya kuzaliwa? Na kama alifurahi au alisikitika ni kwanini?
(a) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni aibu kwa watu waliokuwa
nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika sikukuu yake
(b) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni atakimbiwa na watu
waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika
sikukuu yake
(c) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni si haki na ni uonevu kwa
watu waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika
sikukuu yake
(viii) Baada ya kichwa cha Yohana Mbatizaji kukatwa na kukabidhiwa yule kijana alicheza vizuri mbele ya mfalme Herode, ni wapi alikipeleka hicho kichwa?
(a) mama yake
(b) Kaka yake
(c) Rafiki yake
Friday, July 20, 2012
MECHI MBALIMBALI ZILIZOCHEZWA NA TANZANIA GOSPE TEAM
MECHI KALI KATI YA GOSPEL TEAM NA TUMAINI MEDIA TEAM ZIKIPAMBANA KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA KENTON SINZA MORI
7 March 2012
Mpigaji Picha: Rulea Sanga
Kikosi cha timu ya Gospel
Kikosi cha timu ya Tumaini Media
Refarii Hudson Kamoga akiongea na makepteni kabla ya mechi kuanza
Timu ya Gospel na Tumaini zikiwasalimia kabla ya mechi kuanza
Baadhi ya washabiki wakishuhudia mpambano
Mtangazaji wa Praise Power, Deogras Pius (DP) kulia hakuwa mbali na mpambano.. na siku hii alikuwa daktari wa timu zote mbili
Mfungaji wa goli la kwanza, Gerady (kulia)
Mtangazaji wa Praise Power, Kisaka wa kwanza na anayefuatia ni mtumishi
Stanle kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B
Mwimbaji wa nyimbo za injili Jerry (kulia) na mtangazaji wa Praise
Power Erick Brighton (katikati) na ndiye mratibu wa Gospel Team
akiwacheki wana wakifanya mambo
Add caption
|
Mzee wa Blogu na Creative Director wa kampuni yake inayoitwa Rumafrica
and Africhina, akiwa amepigilia pamba zake za kumtukuza Mungu siku ya
mechi. Na ndiye aliyezipiga hizi picha
Timu ya nje akisubiria kuingia ndani kupiga manyanga
Goalkeeper wa Gospel Team akifanya mambo
---------------------------------------------------------
TIMU YA GOSPEL TEAM YATAMBA KATIKA UWANJA WA SHULE YA SKONDARI KENTON SINZA MORI BAADA YA KUITWANGA TIMU YA VANKHUVA MABAO 5-0
25 Feb 2012
Na mwandishi wenu, Rulea Sanga
Ni siku mbili zimepita, timu ya Gospel Team ilivyopiga bao timu ya
Utumishi wa Umma kutoka ofisi ya Rais-Ikulu mabao 3-2, Jumamosi hii
imegawa dozi tena kwa timu ya Vankhuva kwa kuwapiga mabao 5-0.
Wachezaji wa Gospel team walionekana kuwachanganya wapinzani wake kwa
mbwembwe nyingi uwanjani za kuwapiga chenga na washabiki kuzidi
kuwazingua kwa mavuvuzela.
Baada ya mechi kuisha, makocha wa Gospel Team na Vankhuva Team
waliwasisitiza wachezaji wa pande mbili kukaza buti kimazoezi na
wasibweteke kwa haya mabao 5 na kujiona wamefika mwisho. Wachezaji
waliyapokea hayo kwa mikono miwili na kuahidi kuwa watayatekeleza.
Gospel Team ni timu ambayo inajumuisha waimbaji wa nyimbo za injili,
maproduza na watangazaji wa radio za Kikristo Tanzania. Lengo lao ni
kumuinua Kristo kwa njia ya michezo na kuijenga na kuwaweka fit
wachezaji kiafya. Mbali na hapo ni kujenga urafiki, kujuana na kuinua
vipaji kwa njia ya michezo. Mungu Ibariki Gospel Team
Wachezaji wa Gospel Team wakkimsikiliza mwalimu wao wa mazoezi.
Wachezaji wa Gospel Team wakipasha misuli kabla ya mechi
Timu ya Vankhuva wakiwa tayari kupambana na Gospel Team
Gospel Team ikiwa na sura za mafanikio kabla ya mechi kuanza
Timu ya Vankhuva (jezi ya blue) wakisalimiana kabla ya mechi kuanza
Kazi imenza uwanjani...
MC wa Glorious Celebration hakukosa kuliangalia pambano hili.
Gospel Team wakiwa katika mapumziko kipindi cha kwanza
Mzee wa Mablogu, Rulea sanga (wa pili kushoto) akiwa na goalkeeper wa Gospel Team, Silas Mbise.
Mbali na kuwa na uwezo wa kutengeneza blogu, pia ni mtalaamu wa
shooting, movie editing, Graphic Design, Websites...huyu ni mzee
anayejulika kwa mablogu, Rulea Sanga.
Mratibu wa Gospel Team, Erick (wa tatu kutoka kulia) akitafakari...
Mtumishi kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Stanley
(kushoto), ambaye amekuwa msaada mkubwa katika timu ya Gospel kwa
kuwatibu wachezaji wanaoumia uwanjani.
Fulu kicheko, Mtangazjai na Meneja ya Praise Power Radio ( wa tatu kutoka kushoto) akifuatilia mpambano kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa Vankhuva aliyeumiza baada ya mchezaji wa Gospel team, George Mpela kuvaa kwa bahati mbaya sehemu ya ugoko.
Hiki ni kidonda...Tunaomba maombezi yako kwa huyu mchezaji, kwani ilikuwa bahati mbaya uwanjani
Wachezaji wa pande mbili wakipigwa picha ya pamoja baada ya mechi kuisha
MUNGU IBARIKI GOSPEL TEAM NA VANKHUVA TEAM..AMEN
------------------------------------------------------------------------
BREAKING NEWS
GOSPEL TEAM YA FOOTBALL YAWAPA KIPIGO KILICHOENDA SHULE TIMU YA UTUMISHI WA UMMA KUTOKA OFISI YA RAISI MABO 3-2
WAKATI HUO HUO
TIMU YA NETBALL YA GOSPEL TEAM YAPEWA KIPIGO KITAKATIFU NA TIMU YA
UTUMISHI WA UMMA KUTOKA OFISI YA RAISI MABAO 23-16
MECHI ZILICHEZWA KATIKA UWANJA WA SHULE YA KENTON SINZA MORI TAREHE 23 FEB 2012
Timu ya Utumishi ofisi ya raisi yatoka uwanja huku ikiinamisha vichwa
chini baada ya kupata kipigo kikali kwa kupigwa mabao 3-2 na Gospel
Team. Timu ya Gospel Team ilianza kutikisa nyavu kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa pande mbili walionekana machachari sana vipindi vyote
viwili, kwani kila mmoja alitaka kutoka na ushindi. Mungu alionekana
kuwatetea watoto wake wa Gospel Team kwa kuwapa ushindi.
Mchezaji wa Gospel Team, Elisha alionekana nyota inayong'aa katika uwanja kwa uchezaji wake mzuri.
Wakati huohuo dada zetu wa Gospel team waliabishwa na timu ya Utumishi
wa Umma kutoka ofisi ya Rais baada ya kupata kichapo kitakatifu cha
mabao 23-16. Lakini jina la BWANA linazidi kutukuzwa.
Baada ya Mechi kuisha Gospel Team ilifunga ukurasa kwa nyimbo na maombi makali ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi hilo.
Timu ya Netball kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma kabla ya mech kuanza
Timu ya Netball ya Gospel Team ikiwa katika pozi kabla ya mechi kuanza
Refarii wa katikati akiwapa maelekezo kabla ya mechi kuanza
Kazi imeanza
Timu ya Football ya Gospel Team kabla ya mechi kuanza..Bado wamepiga pamba za mazoezi
Timu kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma akiwa katika pozi kali kabla ya timu kuanza
Watangazaji wa Praise Power Radio, Erick Brighton (kulia), George
Mpella (katikati) na Victor Aron na pembeni yake ni mwanae..wakipasha
kabla ya kuanza mechi
Watangazaji wa Praise Power wakiuangalia mpira waliozawadiwa na mtangazaji wa Clouds FM, George Njogopa
Kazi imenza...maji yametimuliwa
Refarii wetu alikuwa Hudson Kamoga, Mtangazaji wa Praise Power
Goalkeeper wa Gospel Team, Silase Mbise akiwapanga mabeki wake
Baadhi ya wachezaji waliokuwa bench wakiwa na kocha wao (aliyevalia shart la kijani)
Hata mzee wa mablogu, Rulea Sanga (kushoto) alikuwepo uwanjani baada ya
kutoka kijijini kwake Mtili A, Mufindi..angalia akishangaa timu za
mjini...mshamba huyooooooo.....
------------------------------------------------------
TIMU YA WAIMBAJI, MAPROMOTA NA WATANGAZAJI WA RADIO ZA KIKRISTO WAKIWA KATIKA MAZOEZI-SHULE YA KENTON SINZA
Timu hii inafanya mazoezi tayari kupambana na timu mbalimbali ndani ya
jiji la Dar es Salaam na mikoani ndani ya mwezi Februari. Mtapewa
taarifa kwa kupitia blog hiin na kwa kusikiliza Praise Power Radio
99.2FM
Wadada wa Yesu wakifanya mazoezi
Timu imekamilika. hakuna cha wadada wa nani...mambo yanasonga
Dada yetu ambaye jina lake mhalikupatikana akitokea Uganda akifanya mahojiano na meneja wa radio ya Praise Power
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Makondeko akipiga ung'eng'e (kiingereza)
na dada kutokea Uganda aliyefika uwanjani hapo kushuhudia mazoezi
Makondeko mwenye kikaushi cheupe akiutafuta mpiran kwa hamu
Meneja wa Radio ya Praise Power na Mtangazaji, George Mpera akipata matibabu baada ya kuumia mguu
Makondeko akiukimbiza mpira
Kiongozi wa nidhamu wa timu, Noel Tenga akifanya mambo yake katika mtandao wakati wa mazoezi
Mzee wa mablogu na meneja wa kampuni ya RUMAAFRICA & AFRICHINA,
Rulea Sanga, kulia akiwa na marafiki zake (kutoka kushoto ni George
Mpella, rafiki, Erck Brighton)
Wachezaji wakikosoana baad ya mazoezi kuisha
Kiongozi wa timu iliyoko Kinondoni (aliyevaa kofia) akiwaomba wachezaji kufanya mechi na timu yake
--------------------------------------------------------------------------------------------------
WATANGAZAJI, WAIMBAJI NA MAPROMOTERS
WA INJILI TANZANIA WAKIJIFUA TAYARI KUPAMBANA NA TIMU YA BONGO MOVIE
ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI, 28 JANUARY 2012
Mechi hii itachezwa katika viwanja vya TTCL/POSTA Kijitonyama (Science)
ambapo kutakuwa natamasha la uimbaji baada ya mechi kuisha. Waimbaji
kama Bony Mwaitege, Flora Mbasha, Bahati Bukuku, Mzee wa nyimbo ya
zungukazunguka atakuwa ndani ya uwanja, na waimbaji kibao. Kutakuwa na
kiingilio cha buku tano (5000/=) mlangoni, kama utataka tiketi, jisogeze
maeneo ya Efatha Mwenge, Ubungo Oil Com. Mechi itaanza saa 6:00 mchna.
Utakutana na waigizaji wa filamu za Kibongo kama JB, Ray, Kanuba, Irene
Uwoya, Wema Sepetu, na wengine wengi.
Angalia maandalizi haya:
Wtangazaji wa Praise Power Radio, BP (aliyekaa) na Uncle Jimmy wakijadili jambo kabla ya mazoezo kuanza
BIG..George Mpela akipiga kipenga kuwaita wachezaji uwanjani
Fuuuuuuuuulu shangwe na Bony Magupa wa macheliiiiiii...mtangazaji wa Channel Ten
Kiuno kaka..haya yalisemwa na BIG George Mpela (aliyevalia jezi ya yelow...akiwa na mzee wa mablogi Rulea Sanga (RUMA)
"Watumishi hilo zoezi ni noma..sifanyi hata kwa dawa..." Big George Mpella
Majambozi yanendelea
Mtangazaji wa Channel Ten Bony Magupa (kulia) akiwa na Mzee mzima Big-Mtangazaji wa Praise Power, George Mpella..wakitroti....
Kazi inasonga
MAZOEZI YAMEPAMBA MOTO KWA MAPROMOTA,
WATANGAZAJI NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TAYARI KUKABILIA NA TIMU YA
BONGO MOVIE SIKU YA KESHO JUMA JUMAMOSI...
Watangazaji wa Praise Power wakiwa tayari kulianzisha boli
Mchekeshaji Chavala (kulia) akiongea na baadhi ya wachezaji
Wachezaji wakimsiliza kocha wao
Mwimbaji wa nyimbo za injili Bony Mwaitege akiwaweka sawa wachezaji wenzake kwa kuelezea baadhi ya madhaifu aliyoyaona.
Wachezaji wakipata mawaidha kutoka kwa viongozi wao
Blogger Rulea Sanga (alishika mpira) na yeye alikuwapo
Msikilizaji mkubwa wa Praise Power, Mama Abuu akiongea na wachezaji
akiwemo Mtangazaji wa Praise Power Victor Haron (anayevaa soksi)
Kazi inasonga
Mzee wa Mablogi na website na grfix, Rulea Sanga akitoa huduma ya kwanza kwa mtangazaji wa Praise Power, Kisaka.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Musa Shabani akiwa na furaha ya kufa mtuac
Graphic Designer Rulea Sanga akimchua mchekeshaji wa Gospel, Chavala..baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi-------------------------------------------------------------
MECHI KATI YA WATANGAZAJI WA RADIO NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LAFANA KATIKA VIWANJA VYA TTCL- KIJITONYAMA.
Siku iliyokuwa inasubiriwa na Watanzania kuhusiana na mechi kali kati ya
Watangazaji, mapromota na waimbaji wa nyimbo za injili waliotegemea
kupambana na wacheza filamu (Bongo Movie). Zoezi hili halikuweza
kufanikiwa kutokana timu ya Bongo Movie kuwa na mualiko Zanzibar katika
tamasha lao la ZIFF. Badala yake kamati iliamua kupambanisha kati ya
Waimbaji wa nyimbo za injili na Watangazaji wa radio za kikriso
Tanzania.
Tamasha lilionekana kuvutiwa na Watanzania wengi. Timu ya Watangazaji
ilipigwa bao 2 na Waimbaji kuibuka washindi kwa mabao 5. Mfungaji bora
wa watangazaji alikuwa Mtangazaji wa Channel Ten ambaye alikuwa
mtangazaji wa radio ya Praise Power, Boniface Magupa aliyefunga mabao
mawili na kujipatia Tsh. 5000 kama mfungaji bora.
Mbali na mashindano ya mpira ya miguu kulikuwa na mchezo wa kufukuza
kuku ambapo Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore
alijishindia kuku na upande wa watangazaji wa radio, Yusuf Magupa wa
Praise Power alishinda na kujipatia kitoeo cha kuku.
Waimbaji kama Martha Mwaipaja, Martha Ramadhan, Glorious Celebration na
wengine wengi walionekana kugusa mioyo ya watu kwa nyimbo zao zenye
kumwinua Mungu wetu.
Baadhi wa wachezaji wakiwa katika kiwanja cha shule ya Kenton Sinza wakijiandaa kuelekea katika uwanja wa Posta-Kijitonyama.
Stori zikiendelea.....
Timu ya waimbaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Kenton Sinza
Timu ya Watangazaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Shule ya Kenton, Sinza
WACHEZAJI WAKIWA KATIKA UWANJA WA POSTA KIJITONYAMA
Bony Mwaitege (aliyevalia jessy nyeupe) akiufuatilia mpira
Goolkeeper wa watangazaji kutoka radio ya Praise Power, DP akiwa ameshikilia bori baad ya kufungwa.
MC Uncle Jimmy
Kipindi cha kujitambulisha
Mashabiki
Mtangazaji Kisaka
Kipindi cha mapumziko
Timu ya Waimbaji katika kipindi cha mapumziko
Msikilizaji maarufu wa Praise Power a.k.a Mzee wa Kubonya
Mtangazaji wa Praise Power (kulia), Uncle Jimmy na Mchekeshaji Chavala (kushoto)
Mzee wa mblogu na mawebsite pamoja na mgarphics, Rulea Sanga (katikati akiwa amezungukwa na waimbaji wa Glorious Celebration
Mtangazaji wa Wapo Radio, Silas Mbise (kulia) akiwa na rafiki zake. Kutoka kushoto ni Jessica na lilian
Watangazaji wa mpira wakiwa katika corner yao
Waimbakji wa Glorious Celebration wakitoa huduma yao ya juimbaji katika pambalo la mpira
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore (anayepunga mkono), akiwaongoza waimbaji wenzake baada ya kushuka jukwani

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni